March 27, 2017


Manchester City iko tayari kumuuza Samir Nasri hata leo, mwenye fedha nzuri, atangaze ofa.


Wakati City wanaonekana wake tayari kumuachia Nasri, kiungo huyo raia wa Ufaransa ambaye anakipiga katika timu ya Sevilla kwa mkopo, naye ameuza jumba lake lenye thamani ya pauni milioni 5.75.


Jumba hilo la kifahari katika eneo la Cheshire nchini England, tayari limeuzwa kama sehemu ya mkopo na hii maana yake, Nasri hatarejea Man City na inategemea kama Kocha wa Sevilla, Jorge Sampaoli atakuwa anamhitaji, bass atangaze dau.

Nasri alianza kuonyesha uwezo akiwa Arsenal ambayo baadaye ilikubali kumuuza Man City alipoanza vizuri lakini taratibu, akaanza kudorora.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV