March 25, 2017Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amekuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki waliojitokeza kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo.

Mashabiki hao walijitokeza kwenda kuishuhudia Taifa Stars ikipambana na Botswana katika mechi ya kirafiki ambayo walishinda kwa mabao 2-0.

Nape naye aliingia kushuhudia mechi hiyo na mashabiki walimshangilia kwa nguvu wakiimba "Nape, Nape, Nape".

Pamoja na kumshangilia, wengi walikuwa wakigongana kutaka kupiga naye picha naye aliwapa nafasi mashabiki hao.

Baadaye, Nape aliungana na Dk Harrison Mwakyembe ambaye amechukua nafasi yake baada ya kuteuliwa na Rais John Pombe Magufuli.

Nape na Dk Mwakywembe walikaa pamoja na kushuhudia mechi hiyo hadi mwisho.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV