March 25, 2017



Mbwana Samatta ambaye ni nahodha wa Taifa Stars, amesema kweli ali “mmiss” Thomas Ulimwengu katika mechi ya kirafiki dhidi ya Botswana, leo.

Samatta amefunga mabao yote mawili, Stars ikishinda kwa 2-0.

Akizungumza baada ya mchezo, amesema: “Kweli nimemmiss Ulimwengu kutokana na nguvu zake na namna ya kumiliki mpira.

“Lakini kila niliyecheza naye leo, amecheza vizuri sana. Timu nzima inastahili pongezi kwa kucheza vizuri kwa kweli.”

Ulimwengu ambaye anacheza AFC ya Sweden hatuitwa kwenye kikosi cha Stars kutokana na kuwa majeruhi.


Kawaida, Samatta na Ulimwengu walikuwa wakicheza pacha katika kikosi cha TP Mazembe na Taifa Stars pia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic