March 8, 2017





Nahodha wa Mtibwa Sugar, Shabani Nditi, amesema kuwa Yanga wenyewe walijitakia suluhu kwa woga wao wa kumchezesha Kelvin Yondani nafasi ya kiungo namba sita.

Timu hizo, zilivaana wikiendi iliyopita kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro na kumalizika kwa suluhu.

Suluhu hiyo, imeifanya Yanga iendelee kukaa katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 53, huku Simba wakiendelea kuongoza wakiwa na 55.

Nditi alisema Yanga ilikufa kwenye safu ya kiungo kutokana na kumchezesha beki wa kati nafasi ya kiungo na kujikuta muda mwingi wakizuia kuliko kushambulia.

Nditi alisema, katika mechi hiyo umakini mbovu wa washambuliaji wao ndio uliowanyima ushindi kutokana na kutengeneza nafasi nyingi za mabao.

“Wakati timu zinajipanga uwanjani kwa ajili ya kuanza mechi na kumuona Yondani akichezeshwa namba sita, nikajua kabisa Yanga hawatoki salama.


"Kwa sababu Yondani nafasi anayomudu kuichezea vizuri kabisa ni namba tano au nne, lakini siyo sita, hivyo nikajua Yanga wamekuja kulinda goli lao na siyo kushambulia.


"Hivyo, tukatumia udhaifu wa Yanga kwenye safu ya kiungo ambayo ilikufa kwa ajili ya kupeleka mashambulizi golini kwetu, lakini upungufu wa safu ya ushambuliaji tukakosa ushindi katika mechi hii," alisema Nditi.

SOURCE: CHAMPIONI


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic