March 23, 2017Bayern Munich iko katika mapambano ya kisheria na mmoja wa mashabiki wake.

Shabiki huyo amefungua kesi mahakamani akitaka Bayern imlipe kiasi cha pauni 100,000 (zaidi ya Sh milioni 314) baada ya kushambuliwa na mashabiki wa Man United.

Fritz Rettensteiner alikuwa kwenye Uwanja wa Allianz Arena katika mechi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Bayern ilipoikaribisha Man United katika msimu wa 2013-14, hatua ya robo fainali.


Hata hivyo, hakumaliza mechi hiyo baada ya kushambuliwa na mashabiki wa Man United na kukimbizwa hospitali.

Rettensteiner  anaishitaki Bayern kwa kuwa ilishindwa kuweka ulinzi wa uhakika dhidi yake akiwa mteja hadi akakutana na kipigo hicho kilichosababisha hadi leo kutembelea magongo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV