March 23, 2017


Leo usiku huu, Tottenham wanasubiri jibu kuhusiana na kwamba kama inawezekana msimu ujao watumie kwa muda Uwanja wa Wembley.

Uwanja huo unachukua watu 90,000 wakiwa wamekaa vitini na wameomba kuutumia ili kumalizia ujenzi wa uwanja wao mpya.

Tayari ujenzi umeanza na uwanja huo umekuwa ukiukaribia kabisa uwanja wa sasa wa White Hart Lane.

Ili Uwanja mpya wenye uwezo wa kuchukua watu 61,000 uishe ni lazima kipande kikubwa cha White Hart Lane kivunjwe.


Hata hivyo inaonekana wana uhakika wa kulipata jibu hilo.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV