March 23, 2017


Msanii Hamorapa aliamua kutimua mbio baada ya mtu anayedhaniwa ni askari kutoa bastola mbele ya aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Hamorapa anaonekana akimfuata Nape mara tu baada ya kufika katika eneo la nje ya hoteli ya Protea Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Mara baada ya kufika tu, Hamorapa alijisogeza kwa Nape kama alitaka kuzungumza naye lakini mtu huyo aliyeelezwa ni askari alifika na kumtaka Nape alirudi kwenye gari.

Wakati anamtaka ajitambulishe huku akiomba asimsukume, alitoa bastola huku Nape akionekana hana hofu.

Baada ya kuona mtutu, Hamorapa alitimua mbio na kupotelea kusikojulikana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV