March 15, 2017Kiungo wa zamani wa Simba na Yanga, Mganda, Emmanuel Okwi, ameendelea kudhihirisha ubora wake baada ya kuifungia timu yake ya SC Villa mabao matatu.


Mganda huyo, hivi karibuni alijiunga na timu hiyo akitokea Klabu ya SønderjyskE ya nchini Denmark iliyokuwa inashiriki ligi kuu ya nchini huko.

Okwi alifunga mabao katika ushindi wa mabao 4-1 walioupata dhidi ya Onduparaka inayoshiriki Ligi ya Uganda.

Kwa mabao hayo aliyofunga Okwi, ni ishara tosha kuwa ameanza kurudi kwenye kiwango chake cha zamani alichokuwa nacho Simba kabla ya kwenda Denmark.


Baada ya ushindi huo, SC Villa ilipanda kileleni mwa msimamo, katika mechi hiyo, Okwi alianza vibaya baada ya kukosa penalti katika dakika za awali za mchezo huo.Okwi, hadi hivi sasa amefanikiwa kuifungia timu yake ya Villa mabao sita katika michezo mitano aliyocheza tangu atue kuichezea timu hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV