March 26, 2017Vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba leo wameondoka jijini Dar es Salaam kwenda mkoani Kagera.

Simba wanakwenda kucheza na Kagera Sugar mjini Bukoba Aprili 2 ukiwa ni mchezo wao wa kwanza kati ya mitatu wakakayocheza Kanda ya Ziwa.

Baada ya Kagera, Simba watashuka mjini Mwanza ambako watacheza na Mbao FC Aprili 8 na Aprili 12 itakuwa ni dhidi ya Toto African.

Baada ya mechi tatu, Simba watakuwa wamebakiza mechi tatu ambazo kama watashinda zote, wana uhakika wa kubeba ubingwa.


Mechi tatu za Kanda ya Ziwa ndizo zitakazotoa majibu kwa kwa Simba kuwa asilimia ya wao kutwaa ubingwa ni kiasi gani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV