March 26, 2017
Mshambuliaji nyota wa Yanga, Amissi Tambwe ameendelea kupambana na maumivu ya goti lakini sasa ana anafuu.

Tambwe raia wa Burundi ambaye goti limemfanya “apotee” amesema anaendelea vizuri na amekuwa akifanya mazoezi gym.

Akizungumza na SALEHJEMBE, Tambwe amesema amekuwa akisumbuliwa na maumivu makali lakini anashukuru matibabu yamekuwa yakimsaidia.

“Sasa nafuu ipo, nimekuwa naendelea na mazoezi ya taratibu na zaidi nafanya gym. Hapa tunazungumza natokea gym,” alisema.

Tambwe ndiye mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi katika Ligi Kuu Bara ndani ya misimu minne.


Lakini msimu huu unaonekana kuwa mbaya kwake kwani kashindwa kuonyesha cheche hasa baada ya kuandamwa na maumivu hayo ya goti.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV