March 31, 2017




Kampuni kubwa ya ving’amuzi vya kulipia ya StarTimes imepata haki ya kuonyesha moja kwa moja michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika nchini Russia mwaka 2018.

StarTimes itaonyesha michuano hiyo mubasharaa pamoja na uchambuzi wake na itaonyesha katika nchi 42 za Bara la Afrika.

“Tunafurahi kupata haki ya kuonyesha michuano hiyo mikubwa zaidi ya soka duniani ya Kombe la Dunia kwa msimu wote wa 2017-18,” alisema Meneja Masoko wa StarTimes, Felix  Awino.

Maana yake, StarTimes itaonyesha kuanzia hatua zote za awali, kwenda kwenye michuano yenye ya Russia kasoro ile ya Confideration tu.

Awino alisema, lengo kuu la StarTimes  ni kufikisha raha ya mchezo wa soka katika bara la Afrika kwa uhakika zaidi.

Ofisa anayehusika na masuala ya matangazo ndani ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), Philippe Le Floc’h amesema Fifa inajivunia kupata nafasi ya michuano hiyo kuonekana ukanda wa chini ya Jangwa la Sahara ambako StarTimes wataionyesha michuano hiyo.



Nchi 42 ambazo zitafaidika na haki waliyoipata StarTimes , pamoja na Tanzania nyingine ni Angola, Benin, Botswana, Burkina Faso, Burundi, Cameroon, Cape Verde, Central African Republic, Chad, Congo, Congo DR, Côte d’Ivoire, Equatorial Guinea, Eritrea na Ethiopia.

Nyingine ni Gabon, Gambia, Ghana, Guinea, Guinea-Bissau, Kenya, Lesotho, Liberia, Madagascar, Malawi, Mali, Mauritius, Mozambique, Namibia, Niger, Nigeria, Rwanda, Senegal, Seychelles, Sierra Leone, South Africa, Swaziland, Togo, Uganda, Zambia na Zimbabwe..

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic