March 31, 2017


Jesse Lingard sasa ana miezi 18 tu ndani ya kikosi cha Manchester United na mafanikio ya kimaisha yameanza kuonekana.

Umri wake ni miaka 24 tu, tayari sasa anamiliki gari la kifahari aina ya Bentley Continental GT lenye thamani ya pauni 200,000 (zaidi ya Sh milioni 545.2)


Hii inaonyesha kiasi gain mchezo wa soka unavyoweza kulipa. Kama una kipaji ni vizuri kukitumia kwa ajili ya mafanikio.

Kwa wachezaji wa nyumbani Tanzania, inawezekana vigumu kufikia kununua gari la Lingard, lakini soka ni mchezo unaoweza kuwa ajira itakayobadilisha maisha yako. Inategemea kiasi gani uko makini katika kazi yako.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV