March 30, 2017Straika Amissi Tambwe amesema angependa kucheza mechi dhidi ya Azam FC, Jumamosi ndiyo maana amekuwa akipambana kuhakikisha anarejea.

"Napenda sana kurudi na kucheza, hasa mechi dhidi ya Azam. Ninapenda kuisaidia timu yangu. Najua nikiwa fiti nitakuwa msaada," alisema Tambwe ambaye amekuwa akiandamwa na maumivu ya goti kwa zaidi ya wiki mbili.

Tambwe amekuwa akifanya mazoezi gym na mchangani mara baada ya kurejea ingawa ni mazoezi ya taratibu.

Mrundi huyo amekuwa mfungaji bora kwa misimu miwili katika Ligi Kuu Bara katika misimu minne aliyocheza akiwa Simba na baadaye Yanga.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV