March 30, 2017



Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina amesema pamoja na kuandamwa na majeruhi mfululizo, kikosi chake kitakuwa sawa.

Lwandamina amesema washambuliaji wawili wa kati wameendelea kuwa majeruhi kwa kipindi lakini wengine wameendelea kupambana kwa ajili ya timu jambo linawapa moyo zaidi.

Majeruhi ni Donald Ngoma raia wa Zimbabwe na Amissi Tambwe kutoka Burundi ambao wamekuwa tegemeo la ufungaji na kuongoza mashambulizi ya Yanga.

“Tuna wachezaji majeruhi na utaona hawajawa vizuri, mazoezi wameanza lakini si wa kuwategemea. Lakini tunaendelea na maandalizi na wachezaji wengine wanajituma.

“Imani yetu ni kuendelea kupambana na kuimarisha kila sehemu,” alisema.


Yanga imekuwa ikiendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Polisi Kilwa Road jijini Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic