March 22, 2017



Si unajua ule msemo, "utamu hadi kisogoni?" sasa ndiyo mambo yameikuta Simba, ndiyo maana uongozi wa Klabu ya Simba, umesema kwa muda wa wiki moja kikosi chao kukaa mkoani Arusha, umeridhishwa na mandhari ya mji huo ambapo umepanga kurudi kivingine kwa kupiga kambi ya kujiandaa na msimu ujao.


Simba ambayo ilitua mkoani humo Jumatatu ya wiki iliyopita, ilienda kwa ajili ya mchezo wao wa Kombe la FA dhidi ya Madini FC ambapo walicheza Jumapili iliyopita katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid na kuibuka na ushindi wa bao 1-0.


Timu hiyo ambayo ushindi huo umeipeleka hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo, jana Jumanne ilirejea jijini Dar kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao ujao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar.


Makamu wa Rais wa Klabu ya Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’, amesema hawana budi kurejea mkoani humo kutokana na mapokezi na hamasa waliyoipata kutoka kwa Wanasimba wa mkoa huo.


“Kutokana na Wanasimba wa mkoa huu kutupokea vizuri, hatuna budi katika maandalizi yetu ya msimu ujao kuja kuweka kambi huku kwa sababu tumeona ni sehemu ambayo inaweza kukifanya kikosi chetu kupata maandalizi mazuri.

“Kikubwa ambacho naweza kusema, Wanasimba popote pale walipo waendelee kuisapoti timu yao huku tukiwa tunaelekea kutwaa mataji mawili msimu huu, ligi kuu na Kombe la FA,” alisema Kaburu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic