March 22, 2017


Baada ya kikosi cha Azam kuondoshwa kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, kocha mkuu wa timu hiyo, Aristica Cioaba, raia wa Romania, ameweka wazi kwamba hasira zao 

watazimaliza kwenye mchezo wao ujao dhidi ya Yanga.
Azam walitolewa na Mbabane Swallows ya Swaziland baada ya kufungwa mabao 3-0 kwenye mchezo wa marudiano uliopigwa wiki iliyopita nchini Swaziland, hivyo kutolewa kwa idadi ya mabao 3-1.

Mromania amesema kuwa sasa hawana cha kupoteza kwani ni lazima washinde kwenye mechi zao za ligi kuu au kutwaa ubingwa wa Shirikisho (FA), kwa ajili ya kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa.

“Tunataka tushinde mechi zetu zijazo tukianza na Yanga kujihakikishia tunarejea tena kwenye michuano ya kimataifa au kutwaa ubingwa wa FA na kama tukishindwa kufanya hivyo basi ndoto za kushiriki kwa msimu ujao zitafutika.

“Tumeyachukua makosa yetu tuliyofanya kwenye mechi na Mbabane na sasa tunayafanyia kazi yasijitokeze kwenye mechi zijazo na tunaamini kwamba tutashinda kwenye mechi hizo zijazo kwa sababu hatutarudia makosa mara mbili,” alisema Aristica.

Yanga watavaana na Azam kwenye mchezo wa ligi kuu ambao utapigwa Aprili Mosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar ambapo mechi hiyo inatarajiwa kuwa na ushindani kutokana na mfuatano wa timu hizo kwenye msimamo wa ligi.

 Yanga wapo nafasi ya pili wakiwa na pointi 53 na Azam wa tatu na pointi 44, kama Yanga wakipoteza basi mbio zao za ubingwa zinaweza kuwa zimekufa rasmi kwa kuwa Simba wapo kileleni zaidi yao kwa pointi mbili na wakishinda watakuwa wamewazidi pointi tano ikibaki michezo mitano.


1 COMMENTS:

  1. MROMANIA WA YANGA AU AZAM? waandishi fanyeni "proof reading" kabla ya kutuma huu upotoshaji wa habari.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic