March 26, 2017Timu ya Singida imefanikiwa kuwasajili wachezaji wengine Wazimbabwe Elisha Muroiwa mweye umri wa miaka 27 na Wisdom Mtasa 22 kwenye kikosi chao kinachojiandaa na Ligi Kuu Bara.

Katibu Mkuu wa Singida, Abdulrahman Simba alithibitisha hilo kwa kuwasajili nyota hao Muroiwa anayecheza nafasi ya kiungo mkabaji namba 6 ambaye yupo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Zimbabwe iliyokuwa inashiriki Afcon, mwaka huu.


"Ni kweli tumewasajili kabisa leo Singida tumesajili Wazimbabwe wawili mikataba ya miaka miwili ambao ni Muroiwa anayecheza namba 6 aliyekuwepo kwenye timu ya taifa ya Zimbabwe iliyoshiriki Afcon, mwaka huu na Mtasa anayecheza  namba 8 na 10 yeye yupo kikosi cha timu ya taifa cha vijana cha U23,"alisema Sima.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV