March 26, 2017


NYAMAYAO (KULIA) NA BAADHI YA WENZAKE WAKIWA KWENYE FOLENI YA KUINGIA KWENYE UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE (JNIA), LEO.


Watanzania wamepata nafasi ya kufanya kazi nchini China kwa miaka mitatu. Wote hawa ni wasanii wa uigizani. Na kati yao yuko Nyamayao.

Kampuni ya StarTimes Tanzania, jana Jumamosi iliwasafirisha wasanii sita kati ya kumi wa Filamu za Kibongo kwenda China baada ya kupata dili nchini humo.

Wasanii hao ambao wamepata dili la kufanya kazi nchini China kwa miaka mitatu, watakaa huko kwa muda huo wote huku kazi ya kubwa ikiwa ni kutafsiri Filamu za China kwa Lugha ya Kiswahili.


Ikumbukwe kuwa, hivi karibuni jijini Dar, ilizinduliwa filamu ya kwanza ya Kichina iliyotasfiriwa Kiswahili iliyopewa jina la Mfalme Kima.

Kundi la kwanza la wasanii sita lililoondoka juzi ni Rukia Hamdan Suleiman, Safiya Ahmed Said, Hilda Malecela, Abdul Maisara, Abdulrahman Richard na Happiness Stanslaus maarufu kama Nyamayao.

Kundi la pili la wasanii wanne lililobaki, linatarajiwa kuondoka siku yoyote kuanzia leo.


Akizungumza akiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) muda mfupi kabla ya kupanda ndege, Nyamayao aliwashukuru StarTimes.

"Shukurani kubwa kwao, nafasi hii ni kubwa na tuahidi kuifanyia kazi na kuiwakilisha vizuri nchini yetu," alisema.

Nyamayao ni kati ya wasanii waliofanya vizuri wakati wa enzi za mchezo wa "Mambo Hayo" uliokuwa ukirushwa ITV, nyota wengine wakiwa ni akina Bishanga Bashaija, Waridi, Rich Richie na wengine.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV