April 5, 2017


Kocha wa timu ya daraja la tatu nchini Hispania ya Eldense amepandishwa kizimbani kujibu tuhuma za upangaji matokeo.

Eldense ilifungwa mabao 12-0 na FC Barcelona B, lakini kukawa na taarifa za upangaji matokeo.


Baada ya mechi baadhi ya wachezaji walikuwa wakilia huku mmoja akiwatuhumu wenzake kwamba walipanga matokeo.

Kocha na msaidizi wake wamekamatwa pamoja na mchezaji Michael Wayne Fernandez ambaye ni mzaliwa wa England, pia alifikishwa mahakamani akiwa chini ya ulinzi.

Ishu ilikuwa ni kutaka kupata uthibitisho kuhusiana na kipigo hicho kuwa ni kipigo hasa au rushwa.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV