April 11, 2017


Baada ya kupiga bao mbili wakati Simba ikiitwanga Mbao FC kwa mabao 3-2, mshambuliaji Frederic Blagnon amesema anataka kuendelea kufunga mabao zaidi katika mechi zilizobaki.

Blagnon alitokea benchi wakati Simba ikiwa nyuma kwa mabao 2-0, akafunga mawili ya kusawazisha katika dakika ya 83 na 86 na kuiwezesha Simba kuibuka na ushindi huo wa 3-2.

“Nimefurahi kutoa mchango huo kwa timu, lakini nataka kufunga zaidi katika mechi zilizobaki.

“Furaha kubwa ya mshambuliaji ni kufunga mabao, baada ya mabao hayo mawili naona nimeamka. Nataka kufunga tena,” alisema.

Simba ilikuwa nyuma kwa mabao 2-0 hadi katika dakika ya 82 lakini ikapundua kabati kwa kusawazisha yote mawili, kabla ya kufunga la tatu.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV