April 11, 2017



Kikosi cha Yanga kitafanya mazoezi yake ya mwisho jijini Dar es Salaam, leo jioni.

Yanga watafanya mazoezi hayo kabla ya kuondoka kwenda Algeria kuwafuata MC Alger ya Algeria katika mechi ya pili ya Kombe la Shirikisho.

Katika mechi ya kwanza, Yanga iliwavurumisha Waarabu hao kwa bao 1-0 na italazimika kufanya kazi ya ziada kuhakikisha inalinda ushindi huo.

Mazoezi ya mwisho ambayo yatafanyika jijini Dar es Salaam yatakuwa ya mwisho kabla ya Yanga kuanza safari ya kwenda Algeria kesho.


Yanga ndiyo wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa baada ya Azam FC kung’olewa na Mbabane Swallows ya Swaziland.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic