April 18, 2017

HOTELI YA PROTEA DAR.


Huku wapenda soka wakiwa na hamu kubwa kupata majibu kuhusiana na rufaa ya Kagera Sugar kutaka pointi zake, mjadala bado unaonekana kuwa mkubwa ndani ya kamati.

Mahojiano kwa watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa Simba, Kagera Sugar, waamuzi, beki Mohamed Fakhi yanayofanywa na Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) yamekamilika lakini sasa, wajumbe wa kamati hiyo wako katika mjadala wa mwisho.

Waandishi wa habari walio katika hoteli ya Protea Oysterbay wameendelea kusubiri hadi sasa huku kukiwa na baadhi ya wanachama wa Yanga wakiendelea nao kusubiri majibu.

Wote waliotakiwa wameishahojiwa wakiwemo waamuzi wa mchezo kati ya Kagera Sugar dhidi ya African Lyon na sasa kinachosubiriwa ni uamuzi tu.

Tayari kumekuwa na taarifa mitandaoni kuwa Kagera Sugar imeishapewa pointi zake ambazo zilitolewa kwa Simba baada ya kubainika Fakhi alicheza mechi dhidi ya Simba akiwa na kadi tatu za njano lakini Kagera Sugar imesisitiza, ana kadi mbili tu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV