April 18, 2017

Mahojiano kwa watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa Simba, Kagera Sugar, waamuzi, beki Mohamed Fakhi yanayofanywa na Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) yamekamilika.

Wote wameishahojiwa wakiwemo waamuzi wa mchezo kati ya Kagera Sugar dhidi ya African Lyon na sasa kinachosubiriwa ni uamuzi tu.
Kikao hicho kinafanyika katika hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam na Kagera Sugar wamepinga Simba kupewa pointi zao tatu na Kamati ya Saa 72 iliyobaini kuwa Fakhi alicheza mechi dhidi ya Simba akiwa na kadi tatu za njano.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV