April 9, 2017Beki wa kati wa Yanga na nahodha wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema kamwe hawataka tamaa hata kama ushindi wao dhidi ya MC Alger unaonekana ni mwembamba.

Yanga imeishinda MC Alger kwa bao 1-0 katika mechi ya Kombe la Shirikisho iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, jana.

Cannavaro amesema, Yanga bado ina nafasi licha ya wengi kuamini itakuwa imeng’olewa.

“Sisi tunaamini tuna nafasi nna ndiyo maana baada ya mechi ya kwanza, tutaendelea na maandalizi kwa ajili ya mechi ya marudiano,” alisema.


Cannavaro amesema wanaendelea kujiandaa kwa kuwa katika soka, mengi hutokea. Hivyo hawatakata tamaa mapema na wanachojua wana uwezo wa kufanya vema zaidi ugenini. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV