April 12, 2017

NGWENGWE

Kipa wa Mbao, Erick Ngwengwe, amesema aliona mauzauza kwenye mabao matatu aliyofungwa na Simba, juzi.

Simba ilitoka nyuma na kufanikiwa kushinda kwa mabao 3-2 dhidi ya Mbao ya Mwanza kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Katika mchezo huo hadi dakika ya 80 Simba walikuwa nyuma kwa mabao 2-0, lakini wakaamka na kufanikiwa kupata ushindi huo uliowaepeleka kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kuwa na pointi 58, mbili mbele ya Yanga wenye pointi 56.

Ngwengwe ambaye kabla ya kufungwa mabao hayo alikuwa ameonyesha kiwango cha hali ya juu aliliambia Championi Jumatano kuwa mabao hayo hayakuwa ya kawaida.

Kipa huyo amesema kuanza bao la kwanza lililofungwa na Frederic Blagnon hadi la mwisho la Mzamiru Yassin alikuwa hauoni mpira.

“Kwa namna mabao yalivyokuwa yanaingia hata watu waliokuwepo uwanjani naamini walikuwa wanashangaa lakini ukweli ni kwamba kulikuwa na mauzauza japo mtu wa kawaida hawezi kuelewa wala kuamini hali ambayo nilikuwa naiona pale uwanjani.


"Kweli nimeumia sana kwa matokeo tuliyoyapata dhidi ya Simba kwani tulikuwa mbele kwa bao 2-0 lakini kipindi cha pili hasa dakika za mwisho nilianza kuona mauzauza kila ninapotaka kushika mpira hata zile bao ukiangalia zimefungwa katika mazingira ambayo mtu wa kawaida hawezi kuamini," alisema Ngwengwe.

SOURCE: CHAMPIONI

3 COMMENTS:

  1. Hahahahahah ni kasi ya mpira tuu ilimchanganya

    ReplyDelete
  2. Huo ni ushirikina, ashitakiwe Huyo

    ReplyDelete
  3. Magoli yote alijaribu kudaka mpira sasa kama alikuwa haoni kwanini aliendelea kubaki golini?Kipa mwenyewe msomi mwenye shahada ya uzamili anakuja na visingizio so cheap na ajabu waandishi makanjanja hawamuulizi maswali kuhusu madai yake hayo ya kijinga.

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV