Mshambuliaji Danny Usengimana ambaye ameingia wa awali na Singida United, anaelezwa kuwa mshambuliaji hatari zaidi kwa ukanda wa Afrika Mashariki.
Usengimana ambaye anakipiga Polisi Rwanda na alikuwa mfungaji bora, anaelezwa kuwa na kasi, nguvu na mwenye uwezo wa kupiga mashuti makali.
Pia ni mmoja wa washambuliaji hatari kwa kupiga mipira ya vichwa kutokana na umbo lake.
Kabla ya Singida United kumnasa, mshambuliaji huyo amekuwa akiwaniwa na timu kubwa zaidi za Rwanda kama APR na Rayons Sports.
0 COMMENTS:
Post a Comment