April 5, 2017


Wachezaji wa Zenit St Petersburg wakiongozwa na beki wa zamani wa Chelsea, Branislav Ivanovic wameungana na wakazi wa mii wa St Petersburg nchini Russia kuomboleza vifo vya watu 14 waliouwawa kwenye shambulizi la kigaidi.

Watu 14 waliuwawa na zaidi ya 50 kujeruhiwa kwenye shambulizi hilo la bomu kwenye kituo cha chini cha treni.

Shambulizi hilo lilifanywa kati ya miji ya Sennaya Ploshchad na Tekhnologichesky Institut kwenye mii huo wa Petersburg, juzi.

Inaelezwa mtu aliyebeba bimu kutoka Kyrgyzstan ndiye aliyetekeleza tukio hilo.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV