April 6, 2017
Kumekuwa na taarifa kwamba kuna mpango wachezaji wa Yanga wanataka kugoma kwa kuwa hawajalipwa mshahara wa mwezi mmoja.

Lakini Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa alitoa majibu. 

"Nimepata dharula, niko Morogoro nina msiba wa kaka yangu. Kama kweli wataamua kugoma kisa mshahara wa mwezi mmoja na malimbikizo ya deni lao la nyuma binafsi watanisikitisha sana ukizingatia ni mchezo mgumu ambao pia ni mhimu kwao kujitangaza, sitawaelewa kabisa," alisema Mkwasa.

"Iko wazi kabisa kuwa mwenyekiti ambaye alikuwa mdhamini alipatwa matatizo na hadi leo ofisini hajafika. Hata fedha ambazo tunawalipa hawajui wapi huwa tunazitoa. Kuna fedha nyingine tunadai, zaidi ya hapo tufanyeje?

"Tumeshaandaa mchakato wa kufanya harambee ya kuichangia klabu yetu pia kuna hela tunasubiri ambazo zimeshikiliwa na bodi ya ligi, hizo pesa zikitoka basi tumekusudia kuwalipa haraka.

"Suala la kukopa lina taratibu zake au sijui kuweka bondi kuna mambo yake. Sasa tunadaiwa Sh milioni 400 ni pesa nyingi sana hizi.

"Sidhani kama itakuwa sahihi wagombe kwa kuwa hawajalipwa hadi tarehe tano, kuna mashirika hawajalipwa miezi miwili na wanandelea na kazi."


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV