April 6, 2017


Simba imemalizana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) baada ya kulipa zaidi ya Sh milioni 80, kodi ya nyasi bandia zilizo bandarini.

Baada ya hapo, kinachofanyika ni kumalizia masuala kadhaa yakiwepo ya kuzitoa nyasi hizo bandarini.

Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amesema wanaendelea kufuata utaratibu ili kukamilisha na kuzitoa.

“Tayari tumelipa kodi, sasa ni utaratibu wa kuzitoa bandarini ikiwa ni pamoja na malipo ya ziada kwa kuwa nyasi zilikaa bandarini muda mrefu.

“Baada ya hapo, nyasi hizo zitatoka na kitakachofuatia ni suala la kwenda kuzitandaza,” alisema.

“Kabla ya kuzitandaza, mkandarasi atarejea site kwenda kurekebisha mambo kadhaa. Unajua alimaliza muda kidogo lakini hatukuendelea kutokana na suala la nyasi kukwama bandarini.”


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV