April 15, 2017


MABAO ya MC Alger yalipatikana katika muda huu:


DK 14
DK 40
DK 66
DK 90+2


Mpira umekwisha na Yanga imetolewa kwa jumla ya mabao 4-1 baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 jijini Dar es Salaam.

 Mpira ukiwa katika dakika za nyongeza, MC Alger wamepata bao la nne na inaonekana kazi imeisha na matumaini kwa Watanzania, yamefikia mwisho.

MC Alger wamemuingiza Oussama Chita, huyu ni kati ya viungo wakabaji. Inaonekana wanachotaka sasa ni kudhibiti mpira kwa muda mwingi.

Mwinyi anaonekana amechoka, kalambwa kadi ya njano lakini haikuwa faulo ya lazima. Mpira unaonekana kuwa na kasi zaidi kwa MC Alger.

Sasa ni dakika ya 76, Yanga wameamua kumuingiza Mwashiuya kuchukua nafasi ya Ngoma ambaye anaonekana bado hayuko vizuri.

Niyonzima ambaye amepewa kadi ya njano, inaonekana amepunguza  kasi kutokana na kucheza kwa hofu.

MC Alger wamemtia mfungaji wa bao la tatu ambaye ni Bougueche na nafasi yake inachukuliwa Mohammed Seguer, huyu anaonekana ni kinda kabisa. Huenda wanataka kujihakikishia kwa kufunga bao la nne. Lakini wanataka kumiliki mpira ili kuumiliki na kujilinda zaidi.


Hakika hakuna dalili ya matumaini kuwa Yanga wanaweza kusawazisha mabao yote, maana mashambulizi ni machache sana na wanahitaji kubadili aina ya uchezaji.

MC Alger wamepata bao la tatu katika dakika ya 65, Hadj Bougueche ndiye anafunga bao la tatu kwa mkwaju mkali.


Silaha ya Yanga inaonekana kuwa ni eneo la katikati ambako Haruna Niyonzima na Thabani Kamusoko wamekuwa na ushirikiano mzuri.

Pia mabeki wawili wa pembeni, Hassan Kessy na Haji Mwinyi wamekuwa katika kiwango kizuri lakini bado inaonekana nguvu ya ushambulizi ikiongozwa na Donald Ngoma, bado haina nguvu sana.

Sasa ni dakika ya 60, mpira kati ya Yanga na MC Alger unaendelea na wenyeji wanaongoza kwa mabao 2-0.


MC Alger wameonekana kuwa na mashambulizi makali zaidi ukilinganisha na yale ya Yanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV