April 19, 2017



Baada ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), kuiondoa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 ya Mali, kocha mkuu wa timu ya taifa ya vijana ya Tanzania, Serengeti Boys, Bakari Shime ‘Mchawi Mweusi’ amefunguka hawakuwahi kuihofia timu hiyo kutokana na ubora wa kikosi chake.


Mali imeondolewa kushiriki michuano ya vijana inayotarajiwa kuanza kuunguruma Mei 14, mwaka huu nchini Gabon kutokana na migogoro ya kisoka iliyopo nchini mwao iliyosababisha serikali kuingilia kati kinyume na taratibu za Fifa.

Mali ambayo ilikuwa imepangwa Kundi B sambamba na Serengeti Boys, Niger na Angola, baada ya kuondoshwa nafasi yake imechukuliwa na Ethiopia.

Akizungumza moja kwa moja kutoka kambini nchini Morocco, Shime alisema kwa sasa wao wanaendelea vizuri na maandalizi yao huku akisisitiza kuwa kuondolewa kwa timu hiyo hakuwezi kuathiri chochote katika mipango yao.

 “Tunashukuru maandalizi yapo vizuri na kila kitu kipo sawa, vijana wako na ari kubwa kabisa na wako tayari kwa mashindano.                  
     
 “Lakini kuondolewa kwa Mali hakujaathiri lolote kwetu kwa sababu katika maandalizi yetu tunaamini timu zote saba tutakazokutana nazo hakuna rahisi kwani zimefuzu kwa ubora wao,” alisema Shime.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic