April 10, 2017
MPIRA UMEKWISHA
GOOOOOOOOO Dk 90+6  Mzamiru anaachia mkwaju mkali na kufunga bao la tatu
DAKIKA 7 ZA NYONGEZA
GOOOOOOOOO Dk 90+2, Simba wanapata bao la pili baada ya kipa kuukosa mpira, ukamgonga miguu na kumkuta Blagnon ambaye anamalizia kazi
KADI 88 Dk Kotei analambwa kadi ya njano baada ya kucheza undava

DK 86, shambulizi jingine la Simba lakini Blagnon anagongana na kipa, yuko chini anatibiwa
DK 85, mpira wa kurusha wa Bukungu unatolewa na kuwa kona, inachongwa hakuna kitu
GOOOOOOOOO Dk 83, Blagonon anaifungia Simba safi kwa kichwa baada ya kipa kutoka


Dk 82 wanachofanya Simba ni kupeleka mashambulizi haraka, lakini Mbao wanaonekana wametulia zaidi
Dk 81, Blagnon tena anajaribu lakini mpira unaokolewa na kuwa kona, inapigwa hakuna kitu
Dk 79 Blagnon anaachia mkwaju mkali hapa, lakini unatoka sentimeta chache nje
Dk 77, jukwaani kule inaonekana mashabiki wa Simba wanaanza kutoka uwanjani. Kipa wa Mbao alikuwa anatibiwa, ndiyo anainuka

Dk 74 sasa, Simba wameendelea kushambulia mfululizo lakini Mbao wanaonekana ni wazuri zaidi katika ulinzi na nidhamu yao ya ulinzi iko juu
Dk 69, Mbao wanapoteza nafasi nyingine nzuri hapa baada ya mabeki wa Simba kujichanganya
Dk 67 sasa, bado Simba wanafanya mashambulizi mfululizo lakini yasiyokuwa na faida kwao
SUB Dk 60, Liuzio anakwenda nje na nafasi yake inachukuliwa Frederic BlagnonDk 57, Simba wanafanya shambulizi tena na kupata kona
Dk 55 Simba inafanya shambulizi kali hapa, Mo Ibra anaachia mkwaju mkali unaokolewa, Kichuya tena goal kick
Dk 52 Kichuya anapiga vizuri faulo lakini mpira unapiga nyavu za nje
Dk 48, Liuzio anapokea pasi ya nyuma ya Mavugo, anaachia mkwaju mkali hapa, goal kick
KADI Dk 47, Ndemla analambwa kadi ya njano kwa kucheza kibabe
Dk 45, Simba wanaanza kwa kasi hapa na kupeleka mashambulizi. Krosi ya Ndemla lakini hakuna mtu

MAPUMZIKO
DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 44, Kichuya anajaribu anaingia vizuri lakini anashindwa kuutumia mguu wa kulia kupiga krosi
Dk 43 Simba wanapata kona nyingine baada ya shuti la Kotei kumbeba beki Mbao
DK 42, Liuzio anaingia vizuri na kuachia shuti kali, lakini goal kick
SUB Dk 39 anaingia Mavugo kuchukua nafasi ya Hamadi Juma
Dk 36, Kichuya anageuka na kuachia shuti kali kabisa lakini juu
Dk 35, Mbao sasa wanaonekana wamerudi chini na kudhibiti mpira na ulinzi wao unazidi kuwa mkubwa
GOOOOOOOOOOO Dk 33, Benard anapiga shuti kali na kuandika bao la pili kwa Simba ni baada ya counter attack ya maana
SUB SDk 32, anaingia Ndemla kuchukua nafasi ya Pastori
Dk 32, pasi nzuri ya Mo Ibrahim, anaingia vizuri Liuzio inaokolewa nakuwa kona
Dk 28 sasa, hakuna shambulizi lolote kali kwenye lango lolote na inaonekana mpira unachezwa katikati ya uwanja
Dk 25 sasa, inaonekana Mbao FC wako vizuri zaidi ingawa Simba wanajitutumua kupeleka mashambulizi ambayo si makali sana
Dk 22, Simba wanapata kona baada ya kufanya shambulizi. Inachongwa na Kichuya, kona tena

Dk 21, Mbao wanaendelea kulisakama lango la Simba utafikiri ndiyo wako nyuma
Dk 19  Sangija anaingia na kupia shuti kali na kuandika bao safi 
Dk 15, Kichuya anapokea pasi ya Mo Ibrahim, anageuka na kuachia shuti kali
Dk 11, Kotei anaachia mkwaju mkali nje ya 18, goal kick
Dk 8, shuti jingine kali katika lango la Simba, lakini wanaokoa tena

Dk 5, Mbao wanafanya shambulizi kali lakini Zimbwe anafanya kazi ya ziada na kuokoa
DK 1, Mechi imeanza kwa kasi kila timu ikionekana imepania kupata bao la mapema na kujiweka sawa mapema.

2 COMMENTS:

  1. Nawakumbusha tena benchi zima la ufundi mmpeni nafasi zaidi Bragnon ni mchezaji aina ya Drogba wa Chelsea.Tengenezeni combination yake na Mo Ibrahim na Luzio mtaona ukali wake.Pia wanasimba tuwe watu wa kumbukumbu tuwe makini na Aijbu,Banda na Mkude wataiuwa simba mechi za mwisho,nashauri wasipangwe kabisa.

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV