April 11, 2017Furaha ilisababisha Rais wa Simba, Evans Aveva kupoteza fahamu.

Hii ilitokea baada ya Simba kupata bao la tatu katika dakika za nyongeza dhidi ya Mbao FC na kuifanya kuibuka na ushindi wa mabao 3-2.

Simba imeibuka na ushindi huo baada ya Muzamiru Yassini kufunga bao la tatu.

Hadi Mapumziko Mbao FC ilikuwa inaongoza kwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.


Taarifa zinaeleza, Aveva hakutarajia bao hilo na wakati anainuka kushangilia, alipoteza fahamu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV