April 15, 2017




MPIRA UMEKWISHAAA
-LIUZIO ANAACHIA SHUTI lakini hakuna lolote, Toto wanaonekana kupoteza muda
-Kadi YA NJANO KWA HAMIM ABDULKARIM WA TOTO

DAKIKA 5 ZA NYONGEZA
Dk 89, shuti la Mussa katika lango la Simba linaokolewa
Dk 85 Liuzio anajaribu kuachia shuti kwenye msitu wa mabeki wa Toto, kipa anadaka hapa
Dk 83 Toto wanafanya shambulizi jingine lakini ugonjwa ni uleule wa kushindwa kufunga
Dk 80, Bukungu anajaribu kuachia mkwaju mkali hapa lakini goal kick
Dk 76 SUB Juma Liuzio anaingia kuchukua nafasi ya Kichuya anayekwenda benchi
Dk 75 sasa, Toto Africa wanaonekana wana nidhamu ya juu kabisa katika ulinzi kwa kuwa wamejazana kwa wingi
Dk 74 Hussein anamuangusha tena Ajibu nje kidogo ya eneo la 18
Dk 73 mpira wa adhabu ndogo wa Ajibu unagonga mtambaa wa Panya, unarejea uwanjani na Blagnon anapiga kichwa nyanya, Mussa anadaka
KADI Dk 71, Jaffar Mohammed analambwa kadi ya njano kwa kumchezea Ajibu kindava
Dk 68 Junior anapoteza nafasi nyingine tena hapa baada ya kushindwa kulenga lango, Simba wanapaswa kuwa makini kwa kuwa wanaruhusu mashambulizi mengi ya Toto
Dk 64 Junior anapata nafasi nzuri kabisa hapa, hatua moja na lango la Simba anapaisha


Dk 62 Junior anamchambua Zimbwe na kuachia shuti kali lakini Agyei anadaka vizur
SUB Dk 58 Ibrahim Ajibu anaingia kuchukua nafasi ya Laudit Mavugo
Dk 56 Toto wanaingia vizuri tena lakini hawako makini katika umaliziaji
SUB Dk 54, Mo Ibrahim anakwenda benchi na nafasi yake inachukuliwa na Mwinyi Kazimoto
Dk 53, Waziri Junior anashinda kutumia nafasi kwa kuwa Agyei hakuwa langoni
Dk 52, Muzamiru anaachia mkwaju mkali hapa, kipa anadaka unamtoka lakini anawahi

Dk 52 Mo Ibra anaingia vizuri lakini mabeki wa Toto wako makini, wanamdhibiti
Dk 48 Toto wanafanya shambulizi tena lakini Agyei anafanya kazi ya ziada kudaka shuti la Lusajo
Dk 46, Mavugo anaingia hapa, anapiga krosi lakini inawahiwa kwa ulaini kabisa
Dk 46 Blagnon anapata nafasi nyingine, lakini anapiga shuti nyanya
Dk 45 za kipindi cha pili ziemanza na inaonekana Toto Africa ndiyo wameanza na kasi wakilisakama mfululizo lango la Simba


MAPUMZIKO
-Juvenary anaingia vizuri ndani ya lango la Simba, anaachia mkwaju mkali kabisa lakini hakulenga lango -Kipa wa Toto, Mussa yuko chini pale ingawa hakugongana na mtu yoyote
-Kichuya anaachia mkwaju mkuuuuubwaaaaa licha ya kuwa katika nafasi nzuri ya kufunga



DAKIKA 2 ZA NYONGEZA
DK 44 Mavugo anainua krosi safi hapa lakini kipa wa Toto anatoka vizuri na kuiwahi kabla ya kumfikia Blagnon
Dk 43, Kichuya anamlamba chenga beki ndani ya boksi lakini Mussa anawahi na kuokoa, kona. Inachongwa hapa lakini haina manufaa
Dk 40, Zimbwe anaachia krosi ya mpura wa adhabu lakini Blagnon tena, inaonekana alifumba macho, anapiga faulo inayokwenda nje
Dk 38, Simba wanapoteza nafasi nzuri kabisa hapa, Blagnon yeye na kipa wa Toto, anapiga shuti butu tena nje mbali kabsaaaa
Dk 36, krosi ya Junior, mpira unakwenda mikononi mwa Agyei, unamtoka lakini hakuna mtu wa Toto Africa
Dk 35, shambulizi zuri wanafanya Simba, mpira wa kichwa wa beki wa Toto unamkuta Blagnon anaachia mkwaju, gial kick


Dk 31, hakuna ubunifu wa kutosha kutoka kila upande na inaonekana mpira ni ule wa kubutua juu. Hakuna mashambulizi mengi langoni mwa kila timu
Dk 26, Jaffar wa Toto anaachia mkwaju mkali kabisa hapa. Bahati kwa Simba kwa kuwa halikulenga goli. Goal kick
Dk 21, Simba wanacheza mpira wa adhabu, Kichuya anawahi kupiga shuyo lakini kipa Mussa Mohammed, kipa wa Toto anadaka kwa ufundi kabisa
Dk 17, Mavugo anamchambua beki wa Toto, anaingia na kuachia kiki kali lakini goal kick


Dk 16, krosi nyingi nzuri kwenye lango la Simba, Juvenary pastory anaruka na kupiga kichwa kinatoka juu ya lango la Simba.  Toto wanaonekana kufanya mashambulizi mengi zaidi ndani ya dakika 5
Dk 15, Toto wanagongeana vizuri tena na kuingia ndani ya Simba lakini bado umakini katika umaliziaji si mkubwa
Dk 13, krosi safi kabisa kwenye lango la Simba lakini Waziri Junior anachelewa na Simba wanaokoa
Dk 10, Kichuya anaingia vizuri kabisa lakini kipa wa Toto anakuwa makini kabisa


DK 9, walinzi Simba wanaonekana kuzubaa na Waziri Junior wa Toto anaachia mkwaju mkali, lakini ni goal kick
DK 7, Mo Ibra anaingia vizuri na kutoa krosi safi kwa Blagnon lakini anakuwa mzito, anadhibitiwa na kuwa goal kick
KADI Dk 5, Suleiman wa Toto analambwa kadi ya njano kwa kumkwatua Muzamiru
Dk 2 krosi safi ya Bukungu, Kichuya akiwa ndani ya sita anashindwa kufunga na kuwa goal kick
Dk 2 sasa, kinachoonekana kila timu ni kutoondoa wachezaji wanne kwenye safu ya ulinzi. Wanakuwa nyuma 
Dk ya 1, mechi imeanza kwa kasi na Simba wanakuwa wa kwanza kufika katika lango la Toto, hata hivyo Blagnon anafanya madhambi



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic