April 10, 2017
Ndiyo amefikisha miezi mitatu tangu ajiunge na Asante Kotoko ya nchini Ghana, uongozi wa klabu wa hiyo umemfungashia virago aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba Mcroatia, Zradvko Logarussic.

Mcroatia huyo, anatimuwa Asante Kotoko ikiwa ni siku chache tangu mashabiki wa timu hiyo kumvamia kwenye mazoezi ya timu hiyo kwa kile kilichodaiwa kupinga mfumo wa 3-5-2.

Kwa mujibu wa mitandao ya Ghana,  matokeo mabaya ya mfululizo waliyoyapata Asante Kotoko ndiyo sababu ya viongozi kumtimua kocha huyo mwe nye mbwembwe nyingi.

Viongozi wa Kotoko walifikia maamuzi hayo baada ya kikao cha dhararu kilichofanywa jana Jumapili na viongozi wa timu hiyo.

“Mkataba wa Zdravko na klabu umevunjwa rasmi na tayari amepewa taarifa rasmi kutoka kwa uongozi na sasa timu itakuwa chini ya kocha msaidizi, Godwin Ablordey aatakayekaimu nafasi hiyo hadi hapo tutakapotoa taarifa nyingine.
"Maamuzi hayo yametokana na matokeo mabaya ya mfululizo ambayo Katoko wameyapata  kabla ya viongozi kukutana na kujadili mwenendo  wa timu hiyo,"alisema mtoa taarifa huyo.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV