April 8, 2017Nahodha na beki wa kati wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amewatoa hofu mashabiki wa timu yake kuwa wamejipanga kushinda mabao yasiyopungua matatu dhidi ya MC Alger ya Algeria leo.

Leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Yanga inacheza mechi ya kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika na MC Alger ya Algeria.

Cannavaro amesema kuwa: “Tunajua wapinzani wetu ni timu ngumu, lakini tumejipanga kuibuka na ushindi  mkubwa ili tujiweke mazingira mazuri ya kusonga mbele.

“Wapinzani wetu wana historia kubwa na michuano ya kimataifa ngazi ya klabu tofauti na sisi ambao tumekuwa hatufiki mbali, hata hivyo tuna uzoefu na timu za Kiarabu, hivyo tutapambana.


“Tumejipanga kuwafunga hapa nyumbani siyo chini ya mabao matatu kwa sababu itakuwa na faida kubwa katika mchezo wa marudiano.”


Kutokana na mazoezi ya jana asubuhi, kuna uwezekano Cannavaro akaanza kikosi cha kwanza kwa kucheza na Vincent Bossou katika nafasi ya beki wa kati.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV