April 12, 2017


Taarifa kuwa timu zinatakiwa kugoma kuwa kamati ya Saa 72 inaweza kuipa Simba pointi tatu kutokana na kumkatia furaa mchezaji Mohamed Fakhi anayedaiwa alicheza mechi dhidi ya Simba akiwa na kadi tatu za njano.

Masau Bwire msemaji wa Ruvu Shooting, amesema hawana mpango wowote wa kugoma kwa kuwa Ligi Kuu Bara si ya Yanga na Simba.

“Nasikia tu, kwamba tumekubaliana kugoma. Tugome ili iweje? Kwa sababu ipi ya msingi?

“Tuliwahi kuonewa Shinyanga, hakuna Yanga wala Simba aliyetusaidia angalau kuongeza haki zetu. Sasa sisi tunagoma ili iweje?


“Hii si ligi ya Yanga na Simba, hii ni Ligi Kuu Tanzania Bara. Inanishangaza sana lakini naweza kukuambia sisi hatuhusiani na upande wowote, sisi ni Ruvu Shooting tunaojitegemea.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic