April 12, 2017


Mashabiki wa Borussia Dortmund ya Ujerumani, wameonyesha ni waungwana baada ya kuwapa “utelezi” wenzao wa Monaco kutokana na kuvurugika kwa ratiba.


Watoto wa mjini, neno utelezi linatumika kama msaada. Mashabiki wa Dortmund wameamua kuwasaidia wa Monaco wakati timu hizo zinakutana leo mjini Dortmund, Ujerumani.

Mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baina ya timu hizo ilipangwa kufanyika jana, lakini basi la Dortmund likashambuliwa na watu wasiojulikana kupitia milipuko mitatu.

Hali hiyo imefanya Uefa, kusogeza mchezo huo mbele kwa kuwa mchezaji mmoja wa Dortmund, Marc Bartra aliumia na kupelekwa hospitali.

Mashabiki wa Monaco wanatokea nchi jirani ya Ufaransa na Ujerumani ni jirani zao wazuri ambao wameamua kuwaonyesha uungwana huo kwa kuwachukua na kulala nao makwao na kula na kunywa nao pamoja.

Kuvurugika kwa ratiba, kumefanya mashabiki wa Monaco waanze kuhangaika malazi na wale wa Dortmund wameamua kuonyesha mpira ni furaha na wala si uadui, wakawapa utelezi huo safiii.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic