April 4, 2017


Simba wameamua kuelekeza nguvu zao katika mechi za Mwanza.

Ikiwa Mwanza, Simba itacheza na Toto African na Mbao FC.

Mechi hizo inatakiwa kushinda na kutakiwa kurejesha matumaini baada ya kupoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar na kuipa nafasi Yanga kurejea kileleni.

Mmoja wa wajumbe wa kamati ya utendaji ya Simba, ameiambia SALEHJEMBE wameamua kufanya mambo yao kimyakimya.

“Kwa sasa tumeamua kufocus, tunataka kuyapeleka mambo kimyakimya. Lazima turejee katika msitari na kweli tunataka kufanya vizuri.


“Tunaamini bado tuko kwenye njia ya ubingwa, hivyo ni lazima tufanye vizuri hivyo haitakuwa kazi rahisi. Ndiyo maana suala la kuzungumza linakuwa linafuatia baada ya kazi,” alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV