April 4, 2017


 Vijana wa Barcelona B, wameitwanga timu pinzani kwa mabao 12-0.

Barcelona B wameitwanga Eldense kwa idadi hiyo ya mabao na kusababisha wachezaji wake kuanza kuangua kilio.


Eldense walizidiwa kila kitu na kupokea kipigo hicho kikubwa na kusababisha mmoja wao, kuanza kuwalaumu wenzake kuwa “walilamba” mlungula.


Mara ya mwisho katika kiwango hicho cha mabao 12, ilikuwa ni mwaka 1992 baada ya Extremadura  ilipoitwanga Portuense.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV