Abdallah Ameir ambaye ni mwanafunzi kutoka nchini Kenya ambaye anasoma jijini Alger nchini Algeria amesema, lazima wachezaji wa Yanga wajiandae na kelele za mashabiki wa timu ya Mouloudia Club Alger.
Ameir ameiambia SALEHJEMBE kuwa uwanja wa MC Algeri uitwao Omari Hamad unaingiza watu 10,000 tu na mashabiki wakakuwa karibu sana na timu pinzani.
"Mashabiki wanakuwa karibu sana si kama viwanja wa Afrika Mashariki, vingi ni Olimpic Stadium. Kelele ni kubwa sana, halafu wanakuwa wanapuliza moshi na kelele kwa makusudi kama wanashangilia," anasema.
"Aina ya moshi wanaopuliza unakuwa na rangi na kama hujazoea inachanganya. Wachezaji wawekeze nguvu uwanjani kwa kuwa hakuna anayweza kuwaguza. Lakini mashabiki wawe makini sana maana hawachelewi kuwatafutia visa, wakawapiga.
"Wakati wanawashambulia polisi wanajichelewesha kwa makusudi kabisa hadi waone mtu kaumia. Hawa ni watu wasiokubali kushindwa kabisa hasa wanapokuwa kwao."
0 COMMENTS:
Post a Comment