April 11, 2017


Mmoja wa washambuliaji nyota wa MC Alger, Said Ahmed Aouedj amesema aliungalia tofauti mchezo wao dhidi ya Yanga.


Katika mechi hiyo ya Kombe la Shirikisho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Yanga ilishinda kwa bao 1-0.

Aouedj aliyevaa jezi namba 10 katika mechi hiyo na kuingia katika kipindi cha pili, amesema beki Haji Mwinyi ndiye alikuwa hatari zaidi.

"Yanga si timu ya kudharau, wengi walicheza vizuri lakini beki wa kushoto, mwenye nywele za rasta ni "tatizo", ameandika katika ukurasa wake wa Instagram.

Hata hivyo, Aouedj amejigamba safari ya Yanga itaishia nchini Algeria kwa kuwa wana nafasi kubwa ya kuing'oa.

Yanga inatakiwa kupata sare ya aina yoyote au ushindi ili kusonga mbele, jambo ambalo linawezekana kama wakijiamini na kufanya kazi yao kwa mipango sahihi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV