April 25, 2017




Simba imetinga kambini Morogoro na kuwaacha jijini Dar es Salaam wachezaji wake wawili, Jamal Simba Mnyate na Hamadi Juma.

Hamadi Juma aliyejiunga na Simba akitokea Coastal Union ni majeruhi wakati Mnyate amerejea kuwa majeruhi baada ya kuumia tena akiwa mazoezini mjini Bukoba.


Kutokana na hali hiyo, Mnayate na Hamadi wamelazimika kubaki jijini Dar es Salaam.

Kikosi cha Simba ambacho kimeweka kambi mjini humo kujiandaa na mechi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Azam FC.

Mechi hiyo inasubiriwa kwa hamu na wachezaji wa Simba walio kambini hapo wamekuwa wakiendelea na mazoezi.


Simba wamefanya mazoezi leo jioni ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic