April 25, 2017Beki wa Simba, Method Mwanjale wameanza mazoezi taratibu chini ya uangalizi wa daktari.


Mwanjale aliumia na amekuwa nje ya kikosi cha Simba kwa zaidi ya miezi miwili sasa.


Lakini tayari ameanza mazoezi mepesi na Mratibu wa Simba, Abbas Ally ‘Gazza’ amesema kila kitu kinafanyika chini ya uangalizi.


“Daktari ndiye anayesimamia kila kitu, hivyo anajua nini anatakiwa kufanya ingawa ameanza mazoezi chini yake,” alisema Gazza.


Mwanjale yuko Morogoro pamoja na kikosi cha Simba ambacho kimeweka kambi mjini humo kujiandaa na mechi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Azam FC.

Simba imekuwa ikiyumba katika safu yake ya ulinzi kutokana na kumkosa Mwanjale raia wa Zimbabwe ambaye amekuwa tegemeo kubwa wakati akiwa fiti.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV