April 19, 2017Kocha Mkuu wa zamani wa Yanga Mholanzi, Hans Pluijm ambaye sasa hivi yupo Singida United alirejea jijini Dar es Salaam, juzi Ijumaa usiku kwa ajili ya kuanza zoezi zima la usajili wa kikosi chake.


Mholanzi huyo, hivi karibuni alirejea Dar akitokea Ghana ilipokuwa familia yake kwa ajili ya mapumziko mara baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili ya kuinoa Singida.


Kocha huyo, tayari amesajili nyota watatu raia wa Zimbabwe ambao ni Elisha Muroiwa, Wisdom Mtasa wote kutoka Dynamos FC na Tafadzwa Kutinyu aliyekuwa anakipiga Chicken Inn zote za nchini huko.


Pluijm alisema amekatisha mapumziko yake kwa ajili ya kuanza usajili na maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu Bara.


Pluijm alisema, licha ya kuanza usajili wa wachezaji watatu wa kimataifa, lakini bado anahitaji kusajili wachezaji wengine wa kimataifa ili kukamilisha idadi ya wachezaji sita kwa mujibu wa kanuni wa za ligi kuu.


Aliongeza kuwa, pia wamepanga kusajili wachezaji wengine wazawa wenye uwezo na uzoefu wa kucheza mashindano ya ndani na nje ya nchi.


"Nimerejea Dar es Salaam Ijumaa usiku wa saa tatu usiku nikitokea Ghana nilipokwenda kwenye mapumziko ya siku chache mara baada ya kumalizana na Singida.


"Nilikwenda huko kwa ajili ya kuiangalia familia yangu iliyokuwepo nchini huko na kikubwa kilichoniwahisha ni usajili wa wachezaji wapya na maandalizi ya mapema ya msimu mpya.


"Kama unavyojua timu hii ni changa ambayo imepanda kwenye msimu huu ikitokea kwenye daraja la kwanza, hivyo ni lazima nianze maandalizi mapema,"alisema Pluijm.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV