April 19, 2017


Achana na zile habari za hovyo za mambo ya rufaa inayoendelea Bongo, Ulaya ni soka tu na Cristiano Ronaldo ameendelea kuthihirisha yeye ni hatareee baada ya kupiga hat trick wakati Real Madrid ikiitwanga Bayern Munich kwa mabao 4-2 na kutinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Madrid inakwenda nusu fainali kwa jumla ya mabao 6-3 baada ya ushindi wa mabao 2-1 mjini Munich na yote mawili ya Madrid yalifungwa na Ronaldo.


Kwa mabao hayo, maana yake Ronaldo amefikisha mabao 103 aliyofunga katika michuano ya Ulaya ngazi ya klabu. Leo aliingia uwanjani akiwa na mabao 100 baada ya kufunga mawili mjini Munich.

Bayern walianza kufunga bao la kwanza dakika ya 53 kwa mkwaju wa penalti kupitia Robetro Lewandowski, Madrid wakasawazisha dakika ya 76 akifunga Ronaldo kabla ya beki Sergio Ramos kujifunga dakika mbili baadaye.


Kipigo cha 2-1 kwa Madrid kilisababisha kuongezwa kwa dakika 30 na ndipo Madrid ilipoanza kuporomosha mvua ya mabao, Ronaldo akifunga dakika ya 106 kwa pasi ya Ramos na Marcelo akawachambua mabeki wanne kabla ya kumpa pasi safi Ronaldo aliyefunga bao la nne dakika ya 110.

Marco Asensio ndiye aliyefunga bao la nne katika dakika ya 112 na kumaliza kazi dhidi ya Bayern ambao walicheza pungufu kuanzia dakika ya 84 baada ya Arturo Vidal kupigwa “umeme”.


Real Madrid starting XI: Navas; Carvajal, Ramos, Nacho, Marcelo; Casemiro, Kroos, Modric; Isco, Benzema, Ronaldo
Substitutes: Kiko Casilla, James, Kovacic, Lucas Vazquez, Asensio, Morata, Danilo


Bayern Munich starting XI: Neuer, Lahm, Boateng, Hummels, Alaba, Robben, Alonso, Vidal, Thiago, Ribery, Lewandowski 
Substitutes: Ulreich, Bernat, Kimmich, Costa, Rafinha, Coman, Muller













0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic