April 6, 2017
Msanii Roma Mkatoliki, amechukuliwa na watu wasiojulikana na kupelekwa kusikojulikana.

Roma amechukuliwa na watu hao kutoka katika Studio za Tongwe Records zilizo Masaki jijini Dar es Salaam, jana.

Mmiliki wa Tongwe Records, Junior Makame amesema hadi sasa hajui Roma na wenzake wawili walipo.

“Hakika sijui hadi sasa tunapozungumza (saa tano kamili asubuhi). Nimekwenda Polisi Oysterbay, wamesema hawajafika pale.

“Tulijua watakuwa ni Polisi, inawezekana kweli ni wao au la. Lakini hatujui wako wapi ingawa nilielezwa ilikuwa vigumu kujitambulisha.

“Hili si jambo dogo, walifika pale kama saa moja na nusu usiku, waliniulizia mimi na Roma, bahati mbaya mimi sikuwa pale. Hivyo wamewachukua Roma na wengine wawili.

“Sijui wamewapeleka wapi, mbaya pia wamechukua kompyuta na vifaa vingine vya ofisi,” alisema Makame maarufu kama Jay Murder.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV