April 6, 2017


Unaweza kusema mgeni njoo mwenyeji apone, hii inaweza kuwa kauli nzuri ya kuifananisha na namna wenyeji wa Mwanza wanavyoukarabati Uwanja wa CCM Kirumba.

Ukarabati huo ulioanza siku chache zilizopita unatokana na ugeni wanaoutarajia ya mmoja wa vigogo wa soka nchini Simba,
Simba itacheza mechi mbili dhidi ya Mbao FC na Toto African, mechi zinazotarajiwa kuwa na upinzani mkali.

Hivyo uongozi wa uwanja umeona ni wakati mzuri wa kujisahaulisha kusahau kwao na kuanza kufanya ukarabati ikiwa ni pamoja na kuzikata nyasi vizuri.

Huenda baada ya mechi hizo mbili kupita na wenyeji wataanza kufaidi ubora wa uwanja wao ambao waliukosa kabla ya ugeni.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV