April 27, 2017

Kikosi cha Simba chini ya kocha wake, Joseph Omog kimeendelea na mazoezi mjini Morogoro kujiandaa na mechi yao ya keshokutwa ya Kombe la Shirikisho jijini Dar es Salaam.

Simba itakuwa mwenyeji wa Azam FC kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mechi inayotarajiwa kuwa ngumu.

Mratibu wa Simba, Abbas Ally ‘Gazza’, amesema wanaendelea na maandalizi vizuri na uongozi unatimiza majukumu yake kuhakikisha vijana wanafanya vizuri.

“Kila kitu kinakwenda vizuri, kila kitu kipo kamili na hakika vijana wanajituma kweli. Lengo ni kufanya vizuri katika mechi hiyo,” alisema.

“Kila mmoja wetu anajua ni mechi ngumu na muhimu, hivyo kikubwa ni kuendelea kujituma kwa juhudi zaidi.”


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV