Azam FC wameendelea na mazoezi lakini safari hii wamehamia kwenye uwanja nyasi za kawaida na si zile za bandia.
Uwanja huo ni kati ya ile inayomilikiwa na Azam FC kwenye eneo la Chamazi na inaonekana inafanya hivyo ikiwa imelenga kuzoea uwanja huo kwa kuwa itacheza mechi ya Kombe la Shirikisho kwenye uwanja wa nyasi zisizo bandia.
Kawaida, Azam FC hufanya mazoezi yake kwenye uwanja wa nyasi bandia pale Azam Complex, Chamazi.
Azam FC watawavaa Simba katika mechi ya nusu fainali Kombe la Shirikisho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mechi inayotarajiwa kuwa ngumu.
0 COMMENTS:
Post a Comment